Historia
Utangulizi na historia
Tangu ilipoanzishwa mwaka 1997, Sign Industries Ltd imeleta mapinduzi katika bidhaa za mabango na bidhaa zote zinazohusiana na mabango na matangazo katika Tanzania na imetambulisha dhana kadhaa katika tasnia ya mabango ya kisasa kwa Taifa. Neno lililozoeleka wakati huo, lilikuwa "kuandika matangazo" (Sign Writer) ambayo ilifanywa na wasanii ambayo ilikuwa kazi inayojumuisha kuchapa kwenye kibao kwa mkono, useremala, utengenezaji mabangoya mabati
Kuingia kwetu sokoni kuliondoa mitazamo iliyozoeleka katika hatua za utengenezaji ambapo hatua hizo zikafanywa na teknolojia kwa utengenezawaji wa msaada wa kompyuta, (Computer Aided Signs) wakati tulikuwa tumepatwa na msisimko na kujivunia mafanikio yetu, ukweli wa kuhuzunisha tulikuja kutambua kwamba teknolojia imeanza kuchukua nafasi ya wasanii wenye vipaji na mafundi ambao wameridhishwa na kurithi vipaji vikubwa kutoka kwa mabibi na mababu, na hao wasanii na mafundi walikuwa wanakuwa hatarini kuwekwa kando. Kwa jinsi hali hii ilivyokuwa inaendelea kuwa ukweli mchungu na ikawa haiepukiki. Tuliamua kukabiliana na hali ya kusikitisha kwa njia zenye manufaa na kwahiyo tulianzisha programu za mafunzo kwa ajili ya kuvinasa na kuwashirikisha hawa wasanii wa ndani wenye vipaji katika kutumia ujuzi wao pamoja na teknolojia, kwahiyo kuwawezesha kuendelea kuwa hodari na kubaki kwenye biashara kubwa na utenegezaji mkubwa
Matokeo yalikuwa yenye mafanikio makubwa na hatimaye iliirahishishia Sign Industries Ltd ukuaji kwenye nafasi ya kutawala mgao wa soko. Pia tulionyesha dhahiri na kuthibitisha ukweli kwamba wale waliotishwa na utata na kupuuza kuingia kwenye mkumbo wa teknolojia muda si mrefu wangekuwa wamepitwa na wakati na ujuzi wao wa maisha yao yote ungepotea kabisa kwa kuwa nafasi zao kwenye soko zisingeonekana.
Tunaona fahari kusema kwamba tulikuwa waanzilishi kuhusisha teknolojia ya kompyuta katika taratibu zetu na utengenezaji wa bidhaa na mpaka sasa tunaendelea kujiboresha kuendana na teknolojia za kisasa zinazopatikana. Mpaka sasa hivi sisi ni kampuni ya mabango iliyo na vifaa vya teknolojia vilivyo vya kisasa imeajili wabunifu wenye vipaji na teknolojia ya hali ya juu ya kidijitali na mashine za CNC na programu za kompyuta zenye ubora wa hali ya juu.
Kwenye miaka ya mwanzoni ya kuanza kwetu, tuliweza kuleta mabango ya NEON ambayo yalikuwa kitu kipya nchini. NEON ilikuwa changamoto na vilevile ilikuwa fursa na kwa miongo miwili tulikuwa kampuni pekee nchini kutengeneza mabango na alama za NEON. Kwa masikitiko makubwa,mwishoni mwa mwaka 2010 ilitubidi kuacha kutenegeza NEON kwa kuwa ilianza kubadilishwa na mfumo wa mwanga wa LED na hapo tulikuwa watu wa kwanza kuingia kwenye teknolojia hii mpya. Kwahiyo ,mmiliki wa kampuni na wakuu wa kitengo cha uzalishaji walipelekwa Mashariki ya mbali kupata mafunzo ya moja kwa moja kuhusiana na mifumo ya LED na mpaka sasa, mara kwa mara tunahudhuria mafunzo na semina za kimataifa kujiweka kisasa na bidhaa mpya na kiteknolojia.
Tangu kuanzia mwanzo kabisa, tulikuwa na hamu kubwa kuleta mambo mapya katika mabango ambayo yalikuwa siyo tu ya kisasa kwa malighafi bali pia ya kuvutia, yanaendana na hali na nafuu na tulikuwa na nia ya kuongoza sokoni katika masuala ya mabango na kukuza bidhaa na kwa muda mfupi tukatambua kwamba hiyo ndoto ikawa inakuwa kweli. Na kama ukiangalia mabango yetu hapa nchini, tuna matumaini ndoto yetu inatimizwa mbele ya macho yenu wenyewe, na tuna hamu ya kuendeleza mabango yenye mvuto wa ubora kama sehemu ya mfumo wa maisha yetu. Tunajisikia fahari kusema kwamba tumebuni mwenendo mpya katika utamaduni wa makampuni.
Hatuna washindani kwa kuwa tunawachukulia watengenezaji wengine wa mabango kama ni wenzetu katika kugawana soko moja na tunaona fahari kusema kwamba tunatoa msaada wa vifaa na ushauri pale tunapoombwa kufanya hivyo. Lakini kwa hakika ,uzoefu wetu wa muda mrefu na upana wetu na kujiweka kwenye mazingira ya kimataifa na uwezo wa namna nyingi imetupa makali dhidi ya wengine mara nyingi tunaonekana tumewazidi wengine na kuonewa wivu na wengi.
Msingi wa wateja wetu wa sasa ni malai za akaunti za mashirika ikiwa ni pamoja na benki karibu zote makampuni ya mawasiliano, watoa huduma za umma, wasanifu majengo, wajenzi, makandarasi, wajenga majumba, wabunifu na warembaji wa ndani na limepanuka Zaidi ya wamiliki wa biashara za rejareja wa hapahapa na mikoani.
Leo tunachukuliwa kama mamlaka pale inapokuja kwenye mabango na kukuza jina la bidhaa na tumetunukiwa nishani ya juu ya kitaifa ya miradi ya mabango na kupata tuzo za juu 100 za Tanzania kwa mara nane kwa mfululizo na magazeti ya kitaifa na magazeti maarufu yametupa uzito wa makala na kusifia bidhaa zetu kama zina kiwango cha kimataifa
Tutaendelea kuleta mawazo mapya na bidhaa zinazovumbuliwa kwenye tasnia ya mabango ili kuendelea kuboresha utamaduni wa lugha ya mawasiliano ya vielelezo Tupo tayari kuweka wazi kwako siri zetu, uzoefu wetu na mafanikio yetu
Our success is not only because of our internal team work; we also enjoy the teamwork with our clients that adds to the overall experience.